Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya kijana 1 kati ya 6 hana ajira sababu ya COVID-19: ILO

Janga la COVID-19 linaweza kuwa na madhara mengi kwa vijana wafanyikazi-ILO
ILO Photo/Marcel Crozet
Janga la COVID-19 linaweza kuwa na madhara mengi kwa vijana wafanyikazi-ILO

Zaidi ya kijana 1 kati ya 6 hana ajira sababu ya COVID-19: ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Tathimini mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO kuhusu athari za janga la virusi vya corona au COVID-19 imedhihirisha hali halisi ya athari mbaya na kubwa katika ajira ya vijana na pia kuelezea hatua zinazochukuliwa kuhakikisha watu wanarejea salama katika mazingira ya kazi.

Kwa mujibu wa tathimini hiyo ya ILO Zaidi ya kijana 1 kati ya 6 wameacha kufanya kazi tangu mwanzo wa janga la COVID-19 huku wale walioendelea kufanyakazi wameshuhudia saa zao zikipungua kwa asilimia 23.

Tathimini hiyo iloyopewa jina “COVID-19 na ulimwengu wa ajira” inasema vijana ndio walioathirika zaidi na janga hili na ongezeko la kukosa ajira kwa vijana lililoshuhudia kuanzia mwezi Februari linawaathiri wasichana zaidi ya wavulana.

 Mtihani mkubwa kwa vijana

 ILO inasema janga la COVID-19 linanatoa mshituko mara tatu kwa vijana “sio tu kwamba linasambaratisha ajira yao, lakini pia linafuruga elimu na mafunzo na kuweka vikwazo vikubwa katika njia za wale wanaosaka kuingia katika soko la ajira au kuhama kutoka katika kazi moja hadi zingine.”

Kwa mujibu wa ILo asilimia 13.6 ya kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana mwaka 2019 tayari kilikuwa kikubwa kuliko makundi mengine. Kulikuwa na takribani vijana milioni 267 ambao hawakuwa katika ajira, elimu au mafunzo yoyote (NEET) kote duniani.

Na kwa vijana wa umri wa kati ya miaka 15-24 ambao walikuwa wameajiriwa walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa katika mifumo ya kazi ambayo iliwaweka katika hatari kama vile ajira za ujira mdogo, katika seka zisizo rasmi au kama wafanyakazi wahamiaji.

Akizungumzia mtihani huu kwa vijana mkurugenzi mkuu wa ILO, Guy Ryder amesema “Mgogoro wa kiuchumi uliotokana na COVID-19 unawaathiri pakubwa vijana, hasa wanawake kuliko makundi mengine ya vijana. Endapo hatutochukua hatua muhimu na haraka kuimarisha hali yao, kovu litakaloachwa na virusi hivi litakuwa nasi kwa miongo. Endapo vipaji na nguvu ya vinaja itatupwa kando kwa ukosefu wa fursa au ujuzi itaathiri mustakabali wetu wote na kufanya kuwa vigumu zaidi kujikwamua kiuchumi baada ya janga la COVID-19.”

Tathimini hiyo inatoa wito wa haraka  wa kuwa na sera za hatua za kiwango kikubwa kuwasaidia vijana ikiwemo mipango ya kuwahakikishia mafunzo na ajira katika nchi zinazoendelea na program za kina za kuhakikisha ajira katika nchi za uchumi wa kipato cha chini na cha wastani.

 Upimaji na ufuatiliaji unasaidia

 Tathimini hiyo ambayo nit oleo la nne pia inaangalia hatua za kuhakikisha mazingira salama ya kurejea kazini.

Inasema umakini na uhakikishaji wa upimaji na ufuatiliani wa maambukizi ya COVID-19 (TT) vinahusiana kwa kiasi kikubwa na usumbufu mdogo katika soko la ajira n kwa kiasi kikubwa usumbufu mdogo wa kijamii kuliko hatua za watu kujifungia na kusalia majumbani.

Katika nchi zenye uwezo mkubwa kwa kupima na kufuatilia maambukizi kiwango cha wastani cha kupungua kwa saa za kazi kimepunguzwa kwa hadi asilimia 50.

Kuna sababu tatu za hilo kwa mujibu wa tathimini hiyo ambazo ni kwamba TT inapunguza mnepo kuhusu hatua kai za watu kujifungia, inachagiza kujiamini kwa jamii na hivyo kuchagiza matumizi na kusaidia ajira na mwisho kunasaidia kupunguza usumbufu katika mahali pa kazi.

ILO inasema Zaidi ya hayo upimaji na ufuatiliaji wa maambukizi kunaweza kuunda ajira mpya hata kama ni za muda mfupi ambazo zitaelekezwa kwa vijana na makundi mengine yanayostahili kupewa kipaumbele.

Tathimini hiyo imeainisha umuhimu wa kudhibiti faragha ya takiwmu ambayo inatia wasiwasi. Pia gharama ni suala linguine lakini faida za TT katika uwiano ni nzuri zaidi.

Bwana Ryder amesisitiza kwamba “Kuunda ajira bora za kujikwamua na janga hili ambapo pia zinachagiza usawa na uendelevu unaomaanisha kuwafanya wat una makampuni kuweza kufanya kazi tena haraka iwezekanavyo ni sehemu muhimu ya sera endapo tuanataka kupambana na hofu, kupunguza hatari na kuufanya uchumi wet una jamii zetu kuanza tena kuendelea kwa haraka.”

Kupotea kwa saa za kazi

Tathimini hiyo mpya ya ILO pia imetoa takwimu mpya za kupungua kwa saa za kufanyakazi katika robo ya kwanza nay a pili yam waka 2020 ikilinganishwa na robo ya nne ya mwaka 2019.

Makadirio ni kwamba asilimia 4.8 ya saa za kazi imepotea wakati war obo ya kwanza ya 2020 sawa na ajira kamili za kutwa nzia milioni 135 ambazo watu hufanya kwa saa 48 kwa wiki hili ni ongezeko la ajitra milioni 7 tangu lilipotoka toleo la tatu la tathimini ya ufuatiliaji. Na kwa upande wa makadirio ya idadi za ajira zilizopotea katika robo ya pili hayajabadilika yamesalia kuwa milioni 305.

Kwa mtazamo wa kikanda kanda ya nchi za Amerika ni asilimia 13.1, Ulaya na asia ya kati asilimia 12.9