Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Watoto katika kambi ya wakimbizi wa ndani iliyoko Maiduguri, Borno, Nigeria
IOM/Jorge Galindo

Familia za raia wa Nigeria ambao tayari wameathiriwa na migogoro, na sasa COVID-19, ‘wako mahututi’

Msaada na ufadhili vinahitajika haraka kwa mamilioni ya watu nchini Nigeria kwa watu ambao wamepigwa vikali na madhara ya mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19 zikiwemo jamii zinazotegemea misaada kuishi kaskazini mashariki mwa nchi kutokana na migogoro, imesema hii leo ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya dharura, OCHA.

Meli zikiwa katika bandari ya Antwerp
Picha/ IMO

Mabaharia zaidi ya 150,000 wakwama melini sababu ya COVID-19:ILO

Mabaharia wanapaswa kuchukuliwa kama wafanyakazi muhimu hivyo wanastahili kuruhusiwa kurejea nyumbani -limesema leo shirika la kazi duniani ILO, wakati likitoa wito wa hatua za haraka za kuwaachilia mabaharia  kati ya 150,000 hadi 200,000 waliokwama kwenye meli kote duniani kwa sababu ya hatua za kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19.

05 JUNE 2020

Jaridani la Umoja wa Maitafa leo ikiwa Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tutamulika athari za gonjwa la virusi vya Corona katika kulinda wanyama walio hatarini kutoweka.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema tubadili tabia tulinde mazingira kwani muda unayoyoma
-  Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema takribani watu 1,300 ambao ni raia wameuawa katika matukio tofauti nchini DRC. 
- Na shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesaidia raia 179 wa Mali waliokuwa wamekwama Niger.
Sauti
9'57"
Sindano imeandaliwa katika kituo cha umma  cha kampeni ya chanjo huko Sudani Kusini
UNMISS/Tim McKulka

Chanjo ni muhimu lakini pekee haitoshi:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameuambia mkutano wa kimataifa kuhusu chanjo  unaofanyika leo kupitia njia ya mtandao kwamba chanjo ni muhimu sana na imeokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani lakini peke yake haitoshi kukabiliana na majanga makubwa ya kiafya kama linaloisumbua dunia hivi sasa la COVID-19.

Sauti
2'11"