Skip to main content

Vita dhidi ya COVID-19 na utimizaji wa SDGs ni mitihani inayohitaji fedha:UN

Programu za misaada ya chakula nchini Chad zinakuza kilimo endelevu na inaimarisha kipato na riziki.
WFP/Giulio d'Adamo
Programu za misaada ya chakula nchini Chad zinakuza kilimo endelevu na inaimarisha kipato na riziki.

Vita dhidi ya COVID-19 na utimizaji wa SDGs ni mitihani inayohitaji fedha:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo umefanyika leo Alhamisi ukihusisha Umoja wa Mataifa  na maafisa wawakilishi wa serikali mbalimbali, lengo kubwa likiwa ni kuchagiza msaada wa kimataifa wa fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zimedhoofishwa Zaidi na mlipuko wa janga la virusi vya corona au COVID-19 katika katika hatua zake za utumizaji wa malengo ya maendeleo endelevu , SDGs.

Akizungumza katika mkutano huo wa ngazi juu ambao mweyeni ni serikali ya Canada na Jamaica, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Tunapaswa kupambana dhidi ya virusi vya corona huku tukizingatia utimizaji wa SDGs. Hizi ni changamoto na dharura mbili kubwa zinazoikabili jumuiya ya kimataifa. “ Hivyo ameonya kwamba “endapo hatutochukua hatua sasa , janga la COVID-19 litasababisha changamoto isiyoelezeka na madhila makubwa kote duniani.”

Gharama za kutochukua hatua

Kwa mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa gharama za kutochukua hatua zitakubwa mzigo mkubwa kwa nchi zote zinazoendelea na wahisani, njaa isiyotarajiwa na baa la njaa, watu wengine milioni 60 kutumbukia katika ufukara na takribani watu bilioni 1.6 swwa na nusu ya nguvu kazi ya dunia watashindwa kujikimu kimaisha.

Mgogoro wa virusi vya corona pia unaweza kushusha uzalishaji wa dunia kwa dola trilioni 8.5 ambao itakuwa ni upunguaji mkubwa zaidi kuwahi kushuhudia tangu unyogovu wa kiuchumi wa miaka 1930. Hivyo Katibu Mkuu amesema “ni lazima kuhakikisha tunaliepuka hili.”

Guterres ametoa wito kwa mataifa “kukabiliana na janga hili lisilotarajiwa la kibinadamu kwa umoja na mshikamano. Na kipengele muhimu cha mshikamano huo ni msaada wa kifedha.”

Amekumbusha shukran zake kwa shirik ala fedha duniani IMF kwa hatua ambazo tayari limeshazichukua  Pamoja na Benki ya Dunia, benki za kikanda  kwa ajili ya maendeleo, taasisi zingine za kifedha na G20.

 Nchi zinazoendelea haziwezi kushinda COVID-19 peke yao

Katibu Mkuu ameongeza kuwa licha ya juhudi ambazo tayari zimefanyika “nchi nyingi zinazoendelea hazina uwezo wa kupambana na kuishinda corona na kuwekeza katika kujikwamua peke yao “

Hilo limeungwa mkono na waziri mkuu wa Canada Justine Trudeau ambaye ni mmoja wa wenyeji wa mkutano huo . Amesema ingawa nchi yake ni wanachama wa kundi la nchi saba Tajiri zaidi duniani au G-7, Ottawa imebaini kwamba kwamba janga hili limeleta mtihani mkubwa usiotarajiwa na gharama kubwa katika kupambana nalo, kulinda raia wake na changamoto za kujikwamua kiuchumi.

Hivyo amesema “hatuwezi kutarajia nchi ndogo ambazo hazina rasilimali saw ana zetu au miundombinu tuliyonayo na ambazo zinakabiliwa na mazingira magumu Zaidi kuliko yetu zitaweza .”

Ameongeza kuwa ni lazima kutambua ugumu unaozikabili nchi zinazoendelea hasa za afrika nan chi za visiwa vidogo na kusistiza kwamba “Lazima kuwe na hatua za kina na za kudumu za kimataifa kukabiliana na janga hili.”

Rais wa Baraza Kuu

Tathimini hiyo ya waziri mkuu wa Canada imeungwa mkono na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijani Muhammad-Bande ambaye amekumbusha kwamba kabla ya janga la COVID-19 nchi nyingi zilikuwa haziwezi kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs kutokana na matatizo ya kifedha.

Hivyo amesema “Tunapaswa kujikita na changamoto kubwa zinazohusiana na rasilimali fedha ambazo ni lazima zikusanywe sio tu kwa ajili ya kujikwamua haraka lakini pia kwa ajili ya hatua za muda mrefu za kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.”

Kwa mujibu wa Rais huyo wa Baraza Kuu ni Dhahiri kwamba nchi nyingi zinazoendelea hivi sasa hazina uwezo wa kifedha kukomesha kusambaa kwa COVID-19 na athari zake za kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa nchi zilizohatarini zaidi zinakabiliwa na kushuka Zaidi kwa uwekezaji kutoka nje Pamoja na kushuka kwa fedha zinazotumwa kutoka nje , utalii na usafirishaji nje wa bidhaa zao, na usafirishaji haramu wa fedha unaongeza adha kwa mataifa hayo.