Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Msanii na mwanamuziki wa mtindo wa reggae Ziggy Marley alipoahidi kuunga mkono kampeni ya 'Sema ndio kwa watoto' alipotembelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Julai 2001
© UNICEF/Nicole Toutounji

Wimbo maarufu One Love wa Bob Marley kutengenezwa upya ili kuiunga mkono 'Reimagine' ya UNICEF

Wanafamilia wa mwanamuziki nguli na wa kukumbukwa sana duniani, Bob Marley, wametangaza kuutengeneza upya wimbo maarufu wa Bob Marley unaofahamika kwa jina One Love ili waunge mkono kazi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF, kurejesha tena ulimwengu wa haki zaidi kwa watoto ambao maisha yao yamevurugwa na janga la COVID-19, imeeleza taarifa ya UNICEF iliyotolewa hii leo mjini New York Marekani.

08 JULAI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Janga la COVID-19 laongeza usafirishaji haramu wa vifaa tiva visivyokidhi viwango au bandia duniani imesema ripoti iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC

-Nchini Sudan Kusini wapiganaji wa makundi mbalimbali walioletwa pamoja ili kujiunga na mafunzo ya kuingia katika jeshi la kitaifa karibu wanahitimu

Sauti
12'23"
Mkimbizi mwenye umri wa miaka 29 anayetafuta hifadhi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameketi na watoto wake baada ya uchunguzi wa kimatibabu karibu na mpaka wa Zombo, Uganda.
© UNHCR/Rocco Nuri

Wakimbizi raia wa DRC zaidi ya 3,000 wamewasili Uganda ndani ya siku tatu

Zaidi ya wakimbizi 3,000 raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wamewasili Uganda kati ya Alhamis na Ijumaa ya wiki iliyopita yaani Julai 1-3 wakati wa kufunguliwa kwa muda kwa vituo viwili vya mipakani, Galajo na Mlima Zeu, kaskazini magharibi mwa Uganda, limeeleza hii leo mjini Geneva Uswisi, shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi, UNHCR. 

UNICEF/Habib Kanobana

Mwalimu aeleza changamoto za kiuchumi na kijamii kutokana na COVID-19, Uganda

Elimu bora kwa wote ni miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs, lengo ambalo limeingia mashakani kutokana na mlipuko wa COVID-19 kwani serikali nyingi zimelazimika kufunga taasisi za elimu zote kama njia za kuudhibiti. Tuelekee nchini Uganda ambako John Kibego amezungumza na Mwalimu Charles Okuta, mmoja wa walimu waliochaguliwa kutoa mafunzo kwa njia ya redio katika wilaya ya Bwikwe kwa msaada kutoka shirika la World Vision tawi la Bwikwe.

Sauti
3'14"