Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Kwa kawaida mtaa huu wa 42 katika jiji la New York huwa na shughuli nyingi, lakini uliachwa wazi wakati wa janga la CIVID-19
UN News/ Cristina Silveiro

Janga la COVID-19 linatupa fursa ya kuibadilisha miji yetu-Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia ujumbe wake wa uzinduzi wa tamko la kisera kuhusu janga la virusi vya corona katika miji, hii leo ametoa wito kwa viongozi kote duniani kufikiria upya na kurekebisha miji katika kipindi hiki ambacho dunia inapona kutokana na janga la COVID-19 kwani miji imeonekana kuwa kitovu cha janga hilo. 

Sauti
1'43"
UN/ John Kibego

Mustakbali wa wanafunzi wakimbizi wamulikwa kati ya changamoto ya COVID-19, Uganda

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na nchi nyingi duniani kama sehemu ya njia za kudhibiti kuenea kwa COVID-19, zimeathiri vibaya Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs likiwemo lile namba nne linalochagiza fursa za elimu bora. Nchini Uganda, kufungwa kwa taasisi za elimu ni miongoni mwa hatua za kwanza kabisa kuchukuliwa na hatimaye kuathiri moja kwa moja wanafunzi zaidi ya milioni 15. Hata hivyo serikali imetumia mbinu mbalimbali ikiwemo kusambaza masomo kupitia matangazo ya redio na televisheni ambavyo havijaweza kuwafikia wote.

Sauti
3'57"
© UNICEF

Harakati za kupambana na COVID-19 zazidisha machungu kwa wayemen

Nchini Yemen, vita vya wenyewe kwa wenyewe na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, vimeleta taabu kwa wananchi huku familia zikihaha kujinusuru na Umoja wa Mataifa ukiingilia kati kusaidia. Assumpta Massoi anaarifu zaidi.

Hali si shwari nchini Yemen ambako hali ya upatikanaji wa afuta nao si mzuri, madereva katika mji mkuu, Sana’aa wakikesha kusubiri kununua mafuta na hata wakati mwingine baada ya kusubiri muda mrefu mafuta kumalizika kituoni.

Sauti
2'49"
UNOCHA

Guterres: Ulimwengu wa Kiarabu ni wakati wa kugeuza janga la COVID-19 kuwa fursa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Guterres kupitia taarifa ya kisera kuhusu janga la COVID-19 na jinsi ya kujikwamua vyema katika nchi za ulimwengu aloyoitoa hii leo amesema janga hilo limedhihirisha mapungufu na hali tete katika jamii na uchumi duniani kote na ulimwengu wa Kiarabu haukusalimika.

Sauti
2'30"

23 JULAI 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi. Watoto zaidi ya 32 wamepoteza au kutenganishwa na mzazi mmoja au wote kutokana na Ebola tangu kuzuka kwa mlipuko mpya Juni Mosi kwenye jimbo la Equateur Magharibi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Nchini Yemen, vita vya wenyewe kwa wenyewe na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, vimeleta

Sauti
12'51"
IOM/Muse Mohammed

Mmenikirimu nami nalipa fadhila kwa kuwashonea barakoa:Mkimbizi Hamidullah 

Kutana na mkimbizi Hamidullah mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kukimbia machafuko Afghanistan na kupokelewa na kukirimiwa na Kijiji cha Pessat-Villeneuve nchini Ufaransa kwa msaada wa shirika la Umoja wa  sasa analipa fadhila kwa kuisaidia jamii inayomuhifadhi kupambana na janga la corona au COVID-19. John Kibego na maelezo zaidi.

Katika Kijiji kidogo cha Pessat-Villeneuve mkimbizi huyu Hamidullah anasaidia mapambano dhidi ya COVID-19 nchini Ufaransa kwa kutumia ujuzi wake wa ufundi cherahani aliourithi toka kwa mama yake. 

Sauti
1'47"