Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yafuatilia maandamano Iran

UN yafuatilia maandamano Iran

Pakua

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Iran ambako maandamano yanayodaiwa kuwa ni ya kupinga serikali yameingia siku ya tano huku watu 22 wakiripotiwa kuuawa.

Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliulizwa iwapo Katibu Mkuu Antonio Guterres ana kauli yoyote kuhusu kinachoendelea Iran.

(Sauti ya Farhan Haq)

“Katibu Mkuu amekuwa anafuatilia kwa uangalifu maandamano yanayoendelea kwenye miji kadhaa nchini Iran. Tunaelezea masikitiko yetu kufuatia vifo vilivyotokea na twatumia ghasia zaidi zitaepukwa. Tunatumai kuwa haki ya wananchi wa Iran ya kukusanyika kwa amani itaheshimiwa.”

Photo Credit
Farhan Haq, ambaye ni Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/JC McIlwaine)