Kulima tunalima lakini lishe bado ni changamoto tuchukue hatua- Mkulima Sarah
Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.
Mathalani nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO linafadhili mradi wa AgriConnect ambao pamoja na mambo mengine unapatia wananchi, wake kwa waume stadi za mapishi sahihi ya jamii ya mikunde.