Msaada kutoka TANZBATT 10 umenusuru wagonjwa wanaokabiliwa na njaa
Mgeni njoo mwenyeji apone ni methali iliyodhihirisha huko eneo la Mbau jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kikosi cha 10, TANZBATT 10 walipotembelea hospitali ya La Grace kutoa msaada si tu wa chakula bali pia dawa. Walinda amani hawa wanahudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.