Kiwanda cha tiba lishe ni mkombozi kwa watoto wenye unyafuzi Pembe ya Afrika
Nchini Kenya, mfululizo wa misimu mitano bila mvua umeathiri maisha ya jamii zilizo hatarini. Vyanzo vya maji vimekuwa mbali, mimea imekauka, mifugo nayo imekufa. Mambo yote haya yamesababisha watu kutokuwa na uhakika wa kupata chakula, halikadhalika kupungua kwa uzalishaji wa maziwa, bei za vyakula zimepanda, bei za nishati huku uwezo wa watu kununua bidhaa umeporomoka.