Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushiriki wa viongozi wa dini katika kupambana na ukeketaji Tarime Tanzania waanza kuonesha mwanga

Ushiriki wa viongozi wa dini katika kupambana na ukeketaji Tarime Tanzania waanza kuonesha mwanga

Pakua

Ukeketaji unajumuisha taratibu zote zinazohusisha uondoaji wa sehemu au jumla yote ya sehemu ya siri ya nje ya mwanamke. Zoezi hilo mara nyingi hufanywa na waganga wa jadi na wanaokeketa wanajulikana kama mangariba.  Ukeketaji unatambulika kimataifa kama ukiukaji wa haki za binadamu za wasichana na wanawake.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukichagiza mbinu mbalimbali za kutokomeza vitendo hivi vya kikatili na nchi wanachama zimepokea wito huo na kutafuta namba tofautofauti za kupambana na hali hiyo ambayo imejikita katika utamaduni wa baadhi ya jamii ulimwenguni.

Nchini Tanzania katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, viongozi wa dini kutokana na uushawishi wao, wanatumika kujitolea kubadilisha mila hizi zilizopitwa na wakati. Mmoja wa viongozi hao ni Sheikh Shaban Khalfan Mtongori wa eneo la Nyamwaga mjini Tarime anaeleza maoni yake katika mahojiano haya yaliyofanywa na Warren Bright Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu na masuala ya afya ya uzazi, UNFPA Tanzania. 

 

 

Audio Credit
Warren Bright
Audio Duration
3'15"
Photo Credit
UNFPA/ Warren Bright