Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Salvation Youth Group wa Kasulu Kigoma Tanzania waushukuru mradi wa KJP 

Salvation Youth Group wa Kasulu Kigoma Tanzania waushukuru mradi wa KJP 

Pakua

Mnamo mwaka 2017 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO, la Mpango wa Chakula Duniani WFP kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF pia Kituo cha Biashara cha kimataifa ITC, yaliamua kushirikiana kutekeleza mradi wa pamoja Mkoani Kigoma nchini Tanzania, KJP. Kupitia mradi huo unaowahusisha wanawake vijana na wanaume vijana kupitia kwenye vikundi vyao, kikundi cha Salvation Youth Group cha Kasulu Kigoma kimenufaika kwa kupewa mashine ya kutotolesha vifaranga vya kuku kupitia mradi huo. Mwandishi John Kabambala wa Redio washirika KidsTime ya Morogoro, Tanzania, yuko mkoani Kigoma na ameandaa makala ifuatayo.  

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kabambala
Audio Duration
3'21"
Photo Credit
FAO Tanzania