Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutumie elimu tulizonazo kwa vitendo kwa ajili ya ustawi wa jamii zetu – Dkt. Anthony Kiiza 

Tutumie elimu tulizonazo kwa vitendo kwa ajili ya ustawi wa jamii zetu – Dkt. Anthony Kiiza 

Pakua

Ufugaji na kilimo ni moja ya mambo mtambuka ambayo yakifanikiwa yanachangia katika kufanikisha idadi kubwa ya malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kati ya 17 ambayo yanalengwa kufikiwa ifikapo mwishoni mwa muongo huu, mwaka 2030.  

Mathalani lengo namba moja linazungumzia kutokomeza umaskini, namba mbili linaongelea kutokomeza njaa, namba tatu linaongelea afya bora, namba saba linazungumzia nishati bora na ambayo ni nafuu na lengo namba nane likizungumzia ukuaji wa uchumi. Malengo yote hayo yanaguswa moja kwa moja na kilimo.  

Kwa msingi huo, kijana daktari wa mifugo nchini Uganda, Dkt. Anthony Kiiza anasema hajutii kuwekeza katika kilimo na ufugaji kwani hiyo inampa fursa ya kukuza uchumi wake huku akitekeleza utaalamu wake kwa vitendo. Zaidi ya hayo, anahamasisha vijana wenzake kujihusisha na shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ili kukuza uchumi wao na wajamii zinazowazunguka. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amezungumza na kijana huyo katika makala ifuatayo.  

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
Patrick Zachmann/Magnum Photos for FAO