Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sawa Wanawake Tanzania yakabidhi majengo mawili kwa serikali ya Tanzania kusaidia vita dhidi ya unyanyasaji wa watoto

Sawa Wanawake Tanzania yakabidhi majengo mawili kwa serikali ya Tanzania kusaidia vita dhidi ya unyanyasaji wa watoto

Pakua

Mwishoni mwa mwaka jana 2021, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lilisema mwaka huo ulikuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto. Ingawa taarifa ya UNICEF ililenga katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya ni wazi kuwa matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto na unyanyasaji dhidi yao, unaendelea kujidhihirisha katika maeneo mbalimbali duniani. Shirika la Sawa Wanawake Tanzania (SAWA), lililojikita katika kusimamia ulinzi wa mtoto na utoaji elimu jumuishi kwa shule za msingi, linasema limedhamiria kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na ndio maana limeikabidhi serikali ya Tanzania majengo mawili yatakayotumika kama vituo vya kuwahudumia watu waliofanyiwa ukatili katika Halmashauri za Wilaya ya Mvomero na Morogoro. Hamad Rashid wa redio washirika KidsTime ya Morogoro Tanzania ameshuhudia makabidhiano hayo na kutuandalia makala ifuatayo.
 

Audio Credit
Anold Kayanda/Hamad Rashid
Sauti
4'2"
Photo Credit
UN News