Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waendelea kutoa misaada ya dharura Madagascar

Umoja wa Mataifa waendelea kutoa misaada ya dharura Madagascar

Pakua

Kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, nchi ya Madagascar imekabiliana na vimbunga vinne. Jumanne iliyopita, kimbunga Emnati kiliathiri maeno yaleyale yaliyoathirika na kimbunga Batsirai na kuwafurusha makwao maelfu ya watu. Umoja wa Mataifa unashirikiana na wadau wa kibinadamu na serikali ya Madagascar kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura.

Umoja wa Mataifa imetuma pia timu ya dharura ya kutaribu na kutathmini majanga (UNDAC), ikiweka pamoja watalaam wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) na asasi zisizo za kiserikali. Priscilla Lecomte, afisa mawasiliano wa OCHA aliyeambatana na timu hiyo, amezungumza na mmoja wa watalaam hao. 

Audio Credit
Priscilla Lecomte
Audio Duration
2'13"
Photo Credit
© WFP/Sandaeric Nirinarison