Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asasi yetu ya Pwani Teknowgalz inalenga kuwavuta zaidi wasichana katika teknolojia – Aisha Abubakar

Asasi yetu ya Pwani Teknowgalz inalenga kuwavuta zaidi wasichana katika teknolojia – Aisha Abubakar

Pakua

Katika chapisho la mapema mwaka huu la UNESCO kuhusu usawa wa jinsia kwenye utafiti, inaonesha kuwa ijapokuwa idadi ya wanawake kwenye utafiti wa sayansi imeongezeka, bado ni wachache katika nyanja za hesabu, sayansi ya kompyuta, uhandisi na akili bandia. 

Nchini Kenya, wasichana watatu marafiki wamelibaini pengo hilo na wanaendesha asasi waliyoianzisha wakiwa katika masomo ya chuo kikuu ambayo sasa imewanuafaisha takriban wasichana 5000.  Asasi ya Pwani Teknowgalz inawasaidia wasichana kujifunza mambo kadhaa kuhusu taknolojia ya kompyuta na simu. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza  na mmoja wa waassi wa Teknowgalz, Aisha Abubakar ambaye anaanza kueleza historia ya asasi yao hiyo. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'24"
Photo Credit
Picha/Worldreader