Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA na Taasisi ya Panzi DRC yaingia makubaliano kunusuru manusura wa ukatili wa kingono 

UNFPA na Taasisi ya Panzi DRC yaingia makubaliano kunusuru manusura wa ukatili wa kingono 

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamekuwa mwiba siyo tu katika usalama wa taifa hilo bali pia kwa wanawake na wasichana ambao hukumbwa na ukatili wa kingono kule kwenye mapigano. Mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za Umoja wa Mataifa za kuhakikisha manusura wa ukatili huo wanarejeshewa siyo tu utu lakini pia kujiamini na kuendelea na maisha. Miongoni mwa mashirika hayo ni taasisi ya hospitali ya Panzi inayoongozwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dokta Denis Mukwege. Hospitali hiyo iko mjini Bukavu jimboni Kivu Kusini na hivi karibuni ilipata mgeni ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA Dkt. Natalia Kanem ambaye shirika lake linawajibika pia na masuala ya afya ya uzazi na harakati dhidi ya ukatili wa kingono. Assumpta Massoi amefuatilia ziara hiyo na kuandaa makala hii. 

Audio Credit
FLORA NDUCHA/ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
4'57"
Photo Credit
UNFPA/Luis Tato