Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya UNCTAD imenipa motisha zaidi kusaidia jamii – Dkt Julian Omalla

Tuzo ya UNCTAD imenipa motisha zaidi kusaidia jamii – Dkt Julian Omalla

Pakua

Mshindi wa tuzo ya wanawake wajasiriamali iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD na pia akapigwa jeki ya mkopo nafuu wa dola milioni 10 kutoka kwa serikali ya Uganda ameeleza alivyopokea tuzo hiyo na mipango ya baadaye. Akizungumza na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego, Dkt Julian Omalla ambaye amejipatia umaarufu kutokana na shughuli za kujikwamua pamoja na maelfu ya wanawake na vijana, amesema amepata maono makubwa zaidi baada ya kutunikiwa tuzo. Pia ameelezea changamoto lukuki ambazo amekuwa akikumbana nazo tangu mwaka 2012 alipoanzisha upanzi wa miembe wilayani Nwoya. Tayari shamba lake limeleta ajira na matumaini kwa watu zaidi ya 6,000, wengi wakiwa ni wanawake. 
 

Audio Duration
3'42"
Photo Credit
Delight Uganda Limited