Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COUNSENUTH asasi ya kiraia inayotekeleza SDGs Tanzania

COUNSENUTH asasi ya kiraia inayotekeleza SDGs Tanzania

Pakua

Baadhi ya vijiji vya Halmashauri ya Wilaya Chemba mkoa wa Dodoma vimeanza kunufaika na mradi wa visima vya maji safi na salama huku vijiji vingine mchakato wa kuchimba visima ukiendelea. 

Neema hiyo inajiri baada ya asasi isiyo ya kiserikali ya COUNSENUTH inayotekeleza mradi wa Lishe Kijinsia – Dodoma wilayani Chemba katika mkoa wa Dodoma kwa ufadhili wa shirika la msaada la Serikali ya Ireland, yaani Irish Aid. Mradi huu wa Lishe Kijinsia unalengo la kupunguza udumavu kwa watoto kwa kuhusisha mikakati shirikishi ya kuibua na kutatua changamoto za kijinsia zinazoathiri lishe na kuhamasisha mabadiliko ya tabia. 

Suala la maji ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili jamii ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, na hivyo kuwakosesha wanawake muda wa kuhudumia watoto ipasavyo kutokana na kusafiri umbali mrefu kutafuta maji safi na Salama. Hali kadhalika suala la usafi wa mazingira, maji na chakula kwa ujumla.Hadi sasa asasi ya COUNSENUTH imewezesha uchimbaji wa visima katika vijiji tisa kati ya 114 vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ambavyo vitanufaika na mradi huo kwa ufadhili wa shirika la msaada la Serikali ya Ireland, yaani Irish Aid. 

Audio Duration
4'18"
Photo Credit
UNOCHA/Naomi Frerotte