Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Photo/Sophia Paris

Hatua za kupambana na COVID-19 zimeongeza ugumu wa maisha kwa wazee Uganda

Ikiwa leo ni siku ya uelimishaji kuhusu ukatili dhidi ya wazee duniani, tunaelekea nchini Uganda kuangazia hali ya wazee kiafya na kijamii kutokana na vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa COVID-19 ikiwemo kubanwa kwa usafiri wa umma na amri ya kutotembea usiku na hivyo kuongezeka kwa  gharama za kusafiri na uwezo wa kufikia msaada. Maelezo zaidi na mwandishi wetu John Kibego akiwa Uganda.

Sauti
2'34"
UN Photo/Isaac Billy

Nishati ya Ethanol itakuwa mbadala wa mkaa-UNIDO Tanzania

Nishati ya ‘Ethanol’ inayotokana na masalia ya vitu mbalimbali kwa mfano mazao kama miwa, mahindi, viazi na hata ngano ni moja ya suluhisho linaloonekana kuwa mjarabu kwa uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya nishati kama mkaa. Malengo mbalimbali ya maendeleo endelevu SDGs likiwemo lile la 7 linalohamasisha nishati, yanasisitiza uwekezaji katika mbinu mbadala kama hizo za ethanol ili kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi na hivyo kufanikisha  utimizaji wa SDGs ifikapo mwaka 2030.

Sauti
3'43"
UN News/ UN Tanzania

Chuo chetu kimechukua hatua za kujikinga na COVID-19, nasi tunachukua tahadhari zaidi

Katika harakati za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 nchi nyingi duniani zilichukua hatua ya kufunga taasisi za masomo kama shule na vyuo kwa kuwa maeneo hayo huwa na msongamano mkubwa wa watu. Tanzania nayo ilikuwa miongoni mwa nchi zilizochukua tahadhari hiyo hadi pale serikali ilipotangaza kuvifungua vyuo vikuu baada ya kutangaza kuwa sasa hali ya hatari ilikuwa imepungua nchini humo. Je, wanafunzi wanachukua tahadhari gani baada ya kurejea katika mazingira ya masomo?

Sauti
3'10"
Cyril Villemain/UNEP

COVID-19 yaibua changamoto za makazi Uganda

Juhudi za kupambana na COVID-19 zimeibua changamoto mbalimbali na kuathiri vibaya maisha ya watu kiuchumi na kijamii kote duniani. Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Mei, serikali ya Uganda ilichukua hatua ya kufunga fukwe zaidi ya 200 zisizo rasmi kwenye Ziwa Albert zilizo makazi kwa watu zaidi ya 30,000.

Sauti
3'24"
UN Photos

Vichocheo vya mafuriko na atahri zake vyamulikwa nchini Uganda

Juu ya janga la kimataifa la COVID-19, nchi kadhaa Africa Mashariki na Pembe mwa Africa zinakumbana na janga la mafuriko ambalo tayari limewalazimisha wengi kupoteza makazi na hata maisha yao.

Majanga kama hayo huwa na uhusiano na hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Je, mafuriko haya kando na kuathiri binadamu moja kwa moja yana husika vyovyote na shughuli za kiuchumi za binadamu? Basi tuungane na John Kibego aliyevinjari kubaini vichochezi vya mafuriko kwa kufanya mahojiano na mwanamazingira Mosses Semahunge.

 

Sauti
3'25"
UNIC/Stella Vuzo

UNEP inafungua wigo wa watu kuchangia mawazo yao kwa nini wanaona hivi sasa ni wakati wa asili-Clara Makenya

Kesho ni siku ya mazingira duniani, siku ambayo imekuwa ikiazimishwa tangu mwaka 1974 kila mwaka ifikapo tarehe 5 ya mwezi Juni. Siku hii inazihusisha serikali, wafanyabiashara, watu maarufu na wananchi  katika kuelekeza juhudi zao kwenye masuala yanayohusu mazingira hususni yle yanayotishia ustawi wa mazingira yenyewe na matokeo mabaya ya athari hizo. Mwaka huu wa 2020, kauli mbiu imejikita katika baionwai.

Sauti
3'47"
UNDP/Levent Kulu

Watu wengi zaidi watavutiwa kukiwa na miundombinu bora kwa waendesha baiskeli-Abdul Mohamed

Kwa kuthamini upekee kudumu na wepesi wa baiskeli, ambayo imekuwa ikitumika kwa karne mbili hivi sasa, na kwamba ni njia rahisi ya bei rahisi, yenye kuaminika, safi, na inayofaa kwa usafirishaji, kukuza uhamasishaji wa mazingira na afya, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kuidhinisha Juni 3 ya kila mwaka kuwa Siku ya Baiskeli Duniani. Kwa mujibu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO inasisitiza kuwa miundombinu salama kwa waendesha baiskeli ni njia ya kufikia usawa mkubwa wa kiafya.

Sauti
3'53"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

Wanawake walinda amani wana moyo wa uzazi, waje wengi zaidi tupate amani-Mkimbizi Uganda

Wakati ulimwengu ukiwa imeadhimisha siku ya walinda amani duniani maudhui yakilenga wanawake walinda amani ni ufunguo wa amani ya kudumu, Je, wakimbizi nchini Uganda wanasemaje kuhusu shughuli za walinda amani? John Kibego kutoka Uganda amezungumza na baadhi ya wakimbizi akiwemo Dolce Alinda mwanafunzi mjini Hoima na Wilson Katima mwanaharakati wa wakimbizi ambaye pia ni mwalimu wa lugha ya Kiswahili ili kufahamu uelewa wao kuhusu shughuli za walinda amani na hatimaye kumulika haja ya walinda amani wa kike kwenye ujumbe na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa duniani.

Sauti
3'48"