Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuo chetu kimechukua hatua za kujikinga na COVID-19, nasi tunachukua tahadhari zaidi

Chuo chetu kimechukua hatua za kujikinga na COVID-19, nasi tunachukua tahadhari zaidi

Pakua

Katika harakati za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 nchi nyingi duniani zilichukua hatua ya kufunga taasisi za masomo kama shule na vyuo kwa kuwa maeneo hayo huwa na msongamano mkubwa wa watu. Tanzania nayo ilikuwa miongoni mwa nchi zilizochukua tahadhari hiyo hadi pale serikali ilipotangaza kuvifungua vyuo vikuu baada ya kutangaza kuwa sasa hali ya hatari ilikuwa imepungua nchini humo. Je, wanafunzi wanachukua tahadhari gani baada ya kurejea katika mazingira ya masomo? Hawa hapa ni baadhi ya wanafunzi katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma SJMC, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania.

Audio Credit
Loise Wairimu
Audio Duration
3'10"
Photo Credit
UN News/ UN Tanzania