UNEP inafungua wigo wa watu kuchangia mawazo yao kwa nini wanaona hivi sasa ni wakati wa asili-Clara Makenya
Pakua
Kesho ni siku ya mazingira duniani, siku ambayo imekuwa ikiazimishwa tangu mwaka 1974 kila mwaka ifikapo tarehe 5 ya mwezi Juni. Siku hii inazihusisha serikali, wafanyabiashara, watu maarufu na wananchi katika kuelekeza juhudi zao kwenye masuala yanayohusu mazingira hususni yle yanayotishia ustawi wa mazingira yenyewe na matokeo mabaya ya athari hizo. Mwaka huu wa 2020, kauli mbiu imejikita katika baionwai. Clara Makenya ni Mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Tanzania, anaeleza zaidi kuhusu mipango waliyonayo kuiadhimisha siku hii kesho Ijumaa tarehe 5 Juni.
Audio Duration
3'47"