Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nishati ya Ethanol itakuwa mbadala wa mkaa-UNIDO Tanzania

Nishati ya Ethanol itakuwa mbadala wa mkaa-UNIDO Tanzania

Pakua

Nishati ya ‘Ethanol’ inayotokana na masalia ya vitu mbalimbali kwa mfano mazao kama miwa, mahindi, viazi na hata ngano ni moja ya suluhisho linaloonekana kuwa mjarabu kwa uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya nishati kama mkaa. Malengo mbalimbali ya maendeleo endelevu SDGs likiwemo lile la 7 linalohamasisha nishati, yanasisitiza uwekezaji katika mbinu mbadala kama hizo za ethanol ili kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi na hivyo kufanikisha  utimizaji wa SDGs ifikapo mwaka 2030.

Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, amezungumza na Victor Hakim ambaye ni Mratibu wa miradi katika Kitengo cha nishati na mazingira katika shirika la maendeleo ya viwanda duniani UNIDO kuhusu mradi wa shirika hilo wa utengenezaji majiko yanayotumia kemikali ya Ethanol ambayo ni mbadala wa majiko ya mkaa.

Audio Duration
3'43"
Photo Credit
UN Photo/Isaac Billy