Watu wengi zaidi watavutiwa kukiwa na miundombinu bora kwa waendesha baiskeli-Abdul Mohamed

3 Juni 2020

Kwa kuthamini upekee kudumu na wepesi wa baiskeli, ambayo imekuwa ikitumika kwa karne mbili hivi sasa, na kwamba ni njia rahisi ya bei rahisi, yenye kuaminika, safi, na inayofaa kwa usafirishaji, kukuza uhamasishaji wa mazingira na afya, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kuidhinisha Juni 3 ya kila mwaka kuwa Siku ya Baiskeli Duniani. Kwa mujibu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO inasisitiza kuwa miundombinu salama kwa waendesha baiskeli ni njia ya kufikia usawa mkubwa wa kiafya. Mwendesha baiskeli Abdul Mohamed wa Dar es Salaam Tanzania, kupitia mahojiano haya aliyofanyiwa na Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam, anasisitiza suala hilo la miundombinu, lakini kwanza akigusia umuhimu wa siku ya baiskeli duniani.

Audio Credit:
Loise Wairimu/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration:
3'53"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud