Wanawake wa kijijini huko Karagwe mkoani Kagera nchini Tanzania wachukua hatua kulinda tabianchi
Oktoba 15 ni siku ya kuwaenzi wanawake wa vijijini kutokana na mchango wao katika sekta mbalimbali za jamii. Kaulimbiu ya mwaka huu wa 2019 imejikita katika kuangazia jukumu muhimu walilonalo wanawake wa vijijini na wasichana katika kujenga mnepo wa kukabiliana na hali ya hewa. Kulingazia hilo, Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe FM ya mkoani Kagera Tanzania ametembelea kijiji cha Bisheshe na kuzungumza na wanawake walioamua kuendesha kilimo kinachojali mazingira na hali ya hewa.