Kenya tunajitahidi kuwajumuisha wenye ulemavu katika maendeleo-Seneta Mwaura

3 Oktoba 2019

Ujumuishwaji wa kila mtu katika jamii ndio nguzo ya kuhakikisha hakuna ayakayeachwa nyuma katika mchakato wa utimizaji wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu. Umoja wa Mataifa unasema mara nyingi makundi ya walio wachache katika jamii wakiwemo watu wenye ulemavu husahaulika na hivyo imezihimiza nchi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kundi hilo linajumuishwa na kupewa fursa. Miongoni mwa nchi zilizochukua hatua kuhakikisha hilo ni Kenya Ili kufahau kwa undani na ni hatua gani hizo? Flora Nducha katika makala hii anazungumza na Seneta Isaac Mwaura kutoka Kenya ambaye pia ana ualbino. Seneta Mwaura anaanza kufafanua kuhusu hatua hizo.

Audio Credit:
Brenda Mbaitsa/ Flora Nducha/ Isaac Mwaura
Audio Duration:
4'14"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud