Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Nairobi wajitosa kutengeneza majeneza ili  kuinua kipato

Wanawake Nairobi wajitosa kutengeneza majeneza ili  kuinua kipato

Pakua

Katika hatua za kuhakikisha usawa wa kijinsia jamii na wanawake wenyewe wanachukua hatamu kujitosa katika sehemu ambazo kawaida zilizoeleka kuendeshwa na wanaume . Mfano mmoja ni kazi ya useremala hasa ile ya kutengeneza majeneza ambayo kwa kawaida inajulikana kuwa ni kazi wanaume tu. Lakini Joyce Atieno na Eunice Atieno wote wanaoishi mjini Nairobi nchini Kenya, ni kati ya wanawake wachache ambao wamejiunga katika kazi hii na kuifanya kwa moyo wa kujitolea angalau wapate kukidhi mahitaji ya familia zao. Mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya Jason Nyakundi aliwatembelea Joyce na Eunice katika karakana yao iliyo mtaa wa huruma mjini Nairobi kufahamu zaidi kuhusu kazi yao.

 

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Jason Nyakundi
Audio Duration
5'6"
Photo Credit
UN News/ Jason Nyakundi