Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea ICPD 25, Zimbabwe yachukua hatua madhubuti kunusuru vifo vya wanawake na watoto wa kike

Kuelekea ICPD 25, Zimbabwe yachukua hatua madhubuti kunusuru vifo vya wanawake na watoto wa kike

Pakua

Miaka 25 iliyopita huko Cairo Misri nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliazimia kupunguza na hatimaye kutokomeza vifo vya wanawake, wajawazito, watoto wachanga na watoto ili hatimaye dunia hii iwe na ustawi kwa wote bila kujali mtu anaishi eneo gani. Mataifa yalichukua hatua kwa kuzingatia kuwepo kwa mazingira hatarishi si tu kwa mama mjamzito na mtoto anayejifungua bali pia mila potofu na mazingira yanayomuozesha mapema mtoto wa kike na kumnyima haki ya kupata huduma za uzazi wa mpango. Sasa mataifa ikiwemo Zimbabwe yamechukua hatua, je yamefanya nini? Ungana basi na Assumpta  Massoi kwenye makala hii.

Audio Credit
Brenda Mbeitsa
Audio Duration
3'30"
Photo Credit
UNZimbabwe/2018