Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa Mazingira Women Initiative wakijikita katika kuboresha makazi yao Kibera Kenya

Wanawake wa Mazingira Women Initiative wakijikita katika kuboresha makazi yao Kibera Kenya

Pakua

Wakati ulimwengu unaadhimisha siku ya makazi duniani bado mamilioni ya watu wanaishi katika mazingira duni hususan kwenye nchi zinazoendela. Katika mitaa ya mabanda kwa kiwango kikubwa mazingira huwa duni sana.

Mtaa wa mabada wa Kibera au Kibra ulio mjini Nairobi nchini Kenya ni kati ya mitaa mikubwa zaidi ya mabanda duniani. Katika mtaa huo kundi la akina mama lijulikanalo kama Mazingira Women Initiative limejikita katika kuboresha makazi yao kwa kuanzisha mradi wa kuzoa taka na kuzibadlisha kuwa bidhaa muhimu kama mbolea na mifuko. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alizuru mtaa huo wa Kibera kuzunguma na kiongozi wa kundi hilo, Malasen Hamida kufahamu zaidi kuhusu mradi wao.

Audio Duration
4'11"
Photo Credit
Julius Mwelu/UN-Habitat