Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yahaha kulinda mazingira dhidi ya taka ya mafuta

Kenya yahaha kulinda mazingira dhidi ya taka ya mafuta

Pakua

Rasilimali ya mafuta huleta matumaini ya ukuaji wa uchumi wa nchi husika kwani utafutaji, uchimbaji na usafishaji wake huleta fursa nyingi zikiwemo ajira kupitia ukuaji wa viwanda. Lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa  sekta ya mafuta pia  huhatarisha mazingira na afya kutokana na hewa ukaa ya viwandani na taka za mafuta amabyo hujumuisha madini mazito kama zebaki endapo masuala ya mazingira hayashughulikiwi ipasavyo.

Kenya ni nchi ya tatu kugundua mafuta katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Sudan Kusini na Uganda. Bila shaka nchi hiyo kama nyingine inahaha kudhibiti madhara ya mafuta kwa mazingira hasa kutokana na utupaji wa taka za mafuta katika eneo la Turkana ambako wakaazi wameanza kuzihusisha na mambo mengi ikiwemo vifo vya mifugo na harufu mbaya katika kijiji cha Lomokomare na taka ya mafuta kwenye visima vya Twiga. Basi tuungane na John Kibego aliyetembelea vijiji vya Kiturkana na kuandaa makala ifuatayo.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Johh Kibego
Audio Duration
4'3"
Photo Credit
UN News/ John Kibego