Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Nyanduga afarijika na jitihada za Somalia katika haki za binadamu

Awali wiki hii, waziri mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Ali Sharmarke aliliteua Baraza jipya la mawaziri, wakati ambapo Somalia ilikuwa haina serikali tangu Desemba tarehe 6, mwaka 2014.

Hata hivyo, tarehe 20 mwezi Januari, bunge la Somalia limefanikiwa kuridhia mkataba wa haki za watoto, hatua hiyo ikibainiwa na watalaam kama dalili kubwa ya kuonyesha utashi wa serikali katika kuboresha hali ya watoto nchini.

UN Photo/Eskende Debebe

Kumbukizi maalum ya mauaji ya Holocaust

Miaka 70 iliyopita katika kambi ya mateso ya Auschwitz Birkenau majeshi ya washirika yaliyokomboa wafungwa wengi wao wayahudi waliokuwa wanakumbwa na madhila ya kutisha ndani ya kambi hiyo.

Madhila hayo yalitekelezwa na serikali ya kinazi ya Ujerumani. Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa kulifanyika kumbukizi ya tukio hilo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na miongoni mwa waliyojiri ni simulizi kutoka kwa manusura wachache waliobakia hai.

Je nini walisimulia? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii..

Serikali zisituwakilishe , tunahitaji watu wetu kutoka mashinani: Watu asilia

Wakati mkutano wa jukwaa la  wataalamu wa jamii za watu wa asili ukimalizika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini  mjini New York, jamii hizo zinasema kuwa ni dhahiri hazina uwakilishi wa kutosha na mara nyingi erikali za nchi wanakotoka zimekuwa zikiwawakilisha kinyume na matwaka yao.Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mwakilishi wa kundi la wamasai kutoka nchini Kenya ambaye pia anawakilisha taasisi ya ulinzi kwa wasichana ,  ”Keep Girls safe Foundation”  Sein Lengeju anasema licha ya kwamba wmekuwa wakipaza sauti lakini kukosekana kwa uw

UNICEF na kampeni kuhusu haki za watoto

Nchini Tanzania, serikali imekuwa inajitahidi kuendeleza hali ya haki za watoto. Mafanikio hayo yamepongezwa katika mkutano wa 68 wa kamati ya haki za watoto unaoendelea mjini Geneva, Uswisi. Hata hivo, changamoto nyingi bado zipo, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na Mtandao wa Wanahabari Watoto Tanzania limeunda kampeni ya kuelimisha jamii kupitia matangazo ya redio. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Huduma za afya kadhia Uganda

Huduma za afya zimekuwa changamoto kubwa hususani kwa nchi zinazoendelea ambapo wanaothirika zaidi ni wanawake hasa wajawazito wakati wanapojifungua.

Nchini Uganda hali ikoje? Ungana na John Kibego kufahamu kadhia wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo.

Ushiriki wa jamii msingi wa vita dhidi ya umaskini Tanzania

Wakati Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanafikia ukomo mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameanzisha kampeni ya kuelimisha jamii na kushawishi wadau wote ili kuchukua hatua katika kutokomeza umaskini.

Kongamano la kimataifa litakalofanyika mjini New York mwezi Septemba mwaka 2015 linatakiwa kubaini malengo mapya yatakayoongoza shughuli za kupambana na umaskini duniani kwa kipindi cha miaka 15 ijayo.

Harakati za kujikwamua na mimba za utotoni Uganda

Ripoti ya Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA inasema kuwa  Kila mwaka, wasichana Milioni 7.3 wenye umri usiozidi miaka 18 hupata ujauzito na kujifungua. Ripoti hiyo kuhusu hali ya idadi ya watu mwaka 2013, imesema, milioni mbili kati yao hao ni watoto wenye umri usiozidi miaka 14, na kwamba watoto hao hukumbana na matatizo ya muda mrefu ya kiafya na kijamii kutokana na mimba hizo bila kusahau vifo wakati wa kujifungua.

UN Photo/Evan Schneider

Sanaa iliyopigwa marufuku yakumbusha yaliyojiri Auschwitz-Birkenau

Miaka 70 iliyopita, kambi ya Auschwitz-Birkenau huko Poland iliyokuwa ni makazi ya wafungwa wenye asili ya kiyahudi ilikombolewa baada ya madhila yaliyokuwa yanatekelezwa na serikali ya kinazi ya Ujerumani.

Mengi yaliyoendelea kwenye kambi hiyo ikiwemo mateso kwa wafungwa yameendelea kufichuliwa kupitia njia mbali mbali na moja wapo ni onyesho lililoitwa Sanaa iliyopigwa marufuku.

Je ni Sanaa gani na imetumika vipi kufikisha ujumbe wa madhila yaliyokuwa yanatokea kwenye kambi hiyo?.

Ungana na Joshua Mmali kwenye makala hii.

Chupa za plastiki zisizooza zaleta nuru kwa wakazi huko Ufilipino.

Kitendo cha kuwasha taa kwa kubofya tu kiwashio ni jambo ambalo linaonekana ni la kawaida sana kwa baadhi ya watu. Hata hivyo kwa Moja ya Tano ya wakazi wa dunia, matumizi ya taa siyo jambo la kuchagua kwani kwao ni ndoto na hivyo ni maskini wa nishati hiyo ya mwanga. Mathalani nchini Ufilipino, kwa wananchi wanaoishi makazi duni kupata mwanga ni ndoto na kutokana na ujenzi wa makazi yao, giza huwepo hata mchana. Lakini sasa nuru imeingia na ndoto yao sasa imetimia kama ilivyo lengo la mwaka huu wa 2015 ambao umetajwa kuwa mwaka wa mwanga ili kuleta nuru na hatimaye kubadili maisha.