UNICEF na kampeni kuhusu haki za watoto

UNICEF na kampeni kuhusu haki za watoto

Pakua

Nchini Tanzania, serikali imekuwa inajitahidi kuendeleza hali ya haki za watoto. Mafanikio hayo yamepongezwa katika mkutano wa 68 wa kamati ya haki za watoto unaoendelea mjini Geneva, Uswisi. Hata hivo, changamoto nyingi bado zipo, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na Mtandao wa Wanahabari Watoto Tanzania limeunda kampeni ya kuelimisha jamii kupitia matangazo ya redio. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Photo Credit
Wanahabari watoto Tanzania wakiandaa habari zinazohusu watoto. Picha@UNICEF