Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyanduga afarijika na jitihada za Somalia katika haki za binadamu

Nyanduga afarijika na jitihada za Somalia katika haki za binadamu

Pakua

Awali wiki hii, waziri mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Ali Sharmarke aliliteua Baraza jipya la mawaziri, wakati ambapo Somalia ilikuwa haina serikali tangu Desemba tarehe 6, mwaka 2014.

Hata hivyo, tarehe 20 mwezi Januari, bunge la Somalia limefanikiwa kuridhia mkataba wa haki za watoto, hatua hiyo ikibainiwa na watalaam kama dalili kubwa ya kuonyesha utashi wa serikali katika kuboresha hali ya watoto nchini.

Katika mahojiano yafuatayo na Priscilla Lecomte, Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia, Tom Bahame Nyanduga, anaeleza Redio ya Umoja wa Mataifa matumaini yake kuhusu mabadiliko yanayotokea nchini Somalia.

Photo Credit
Tom Bahame Nyanduga, Picha ya UN/Jean-Marc Ferré