Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Graca Machel na harakati dhidi ya ndoa za mapema, ukeketaji na haki za wanawake nchini Tanzania

Graca Machel na harakati dhidi ya ndoa za mapema, ukeketaji na haki za wanawake nchini Tanzania

Pakua

Mapambano dhidi ya ndoa za mapema,  ukeketaji kwa lengo la kuimarisha haki za wanawake kwa ujumla yamechukua sura mpya nchini Tanzania pale mwanaharakati wa haki za wanawake ambaye pia ni mjane wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Graca Machel alipofanya ziara maalum nchini humo. Hii ni ziara iliyoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA ambayo  iliyomkutanisha Bi Graca na watunga sera, mashirika ya haki za wanawake na taasisi mbalimbali, wanawake wenyewe pamoja wadau mbalimbali wa haki za wanawake na kuliangazia barabara suala la ndoa za umri mdogo na ukeketaji na masuala mengine yanaohusiana na haki za wanawake.Bi Graca akiambatana na maafisa kutoka UNFPA na wadau wengine, walisafiri hadi mkoani Mara mkoa ambao kwa mujibu wa takwimu za UNFPA ni kinara wa ukeketaji na ndoa za mapema. Je nini kilijiri? Basi kwa kina ungana na msimulizi wetu….

Photo Credit
Wasichana waliopokea mafunzo nchini Tanzania(Picha ya UNFPA / Zainul Mzige)