Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mtama waimarisha usalama wa chakula India.

Kwa kipindi kirefu nchiniIndiamazao ya mchele na ngano yamekuwa yakipewa kipaumbele, hata hivyo wakulima hawajafanikiwa kupitia mazao hayo. Lakini sasa ziko habari njema kwa wakulima hususani ni wa zao la mtama ambalo huemda likanufaisha nchi na hata kusaidia katika usalama wa chakula.

Ungana na Grace Kaneiya kwa undani wa ripoti hii.

Amani usalama, maendeleo vyamulikwa New York

Warsha ya tatu ya muundo wa Umoja wa Mataifa inayohusisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali duniani imeanza mjiniNew York, ambapo wanafunzi hao wamesema watayatumia mafunzo kama nyenzo  ya kukuza amani usalama na maendeleo.

 Ungana na Joseph Msami aliyefanya mahojiano na wawakilishi wa Kenya na Tanzania katika warsha hiyo.

UN Women yasaidia majaji wanawake Tanzania kuelimisha umma juu ya rushwa ya ngono

Siku hizi majaji, mahakimu, maafisa wa polisi na askari magereza nchini Tanzania wamekuwa wakijitahidi kuelimisha umma juu ya kutokomeza rushwa ya ngono. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women, katika kuchochea elimu hiyo hivi karibuni lilifadhili chama cha majaji wanawake Tanzania, TAWJA kuandaa kitabu kuelimisha umma na mafunzo juu ya rushwa ya ngono. Mafunzo hayo ni pamoja na  yale yaliyofanyika kwa siku mbili huko Arusha na Mwanza.

Ujasiriamali sasa unawezekana Nepal

Kukuwa kwa biashara ndogo ndogo ni ndoto ambayo imeanza kutimia nchini Nepal baada ya muda mrefu. Mchakato huu ulikwamishwa na mkwamo wa kiteknolojia na sababu kadhaa. Ungana na Flora Nducha katika makala ifuatayo inayofafanua mapambazuko mapya nchini humo.

Wakimbizi wa Syria wamiminika Iraq

Wakimbizi wa Syria walioko Iraq wanaendelea kuongezeka kila uchao. Wengi wao wakisema wanakimbia machafuko yanayoendelea kati ya vikundi vyenye silaha . UNHCR imesema Mmiminiko huu umepelekea upungufu wa Chakula, maji na umeme basi ungana na Joseph Msami katika ripoti hii