Wahamiaji wa Kiethiopia na Kisomali wakwama Yemen IOM yaomba msaada
Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Djibouti limetoa ombi la dharura la dola Milioni Tano kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahamiaji wa Ethiopia na Somaliawalio kwenye mazingira magumu nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari ya ughaibuni.
Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema ombi la awali la dola Milioni 72 kwa Djibouti kupitia mchakato wa Umoja wa Mataifa bado halijatekelezwa na sasa wanahitaji haraka fedha hizo kukwamua wahamiaji hao walio kwenye ofisi ya IOM huko Obok nchini humo.