Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Biashara ya hewa ya ukaa bado kitendawili, gesi chafuzi zinazidi na umaskini ni kikwazo: Tanzania

Tanzania inaendelea na jitihada za kupunguza makali yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi wakati huu ambapo jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa linalojadili mabadiliko ya hali ya hewa IPCC limetoa ripoti kwamba shughuli za binadamu ndio chanzo kikuu cha mabadiliko hayo. Je Tanzania imefikia wapi? Na vipi biashara ya hewa ya ukaa?

Hayo na mengineyo aliulizwa Waziri husika wa mazingira wa Tanzania Dkt. Tereziya Huviza katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Hata baada ya 2015 tuna wajibu wa kutimiza malengo yaliyosalia:Mwinyi

Waziri wa afya wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi amesema pamoja na serikali ya Tanzania kutimiza lengo la nne la milenia ambalo ni kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano, taifa hilo bado lina wajibu wa kuhakikisha malengo mengine yaliyosalia yanatimizwa hata baada ya ukomo wa malengo hayo mwaka 2015.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Mwinyi amesema wamewasilisha mapendekezo yao kwenye baraza kuu ya kutana kutimiza malengo yaliyosalia na pia kuunda malengo mapya. Ameketi na Flora Nducha kufafanua yote hayo akianza na malengo yahusuyo afya

Uganda yahaha kunusuru mazingira

Utunzaji wa mazingira ni miongoni mwa malengo manane ya maendeleo ya milenia yanayojadiliwa katika mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, ili kutathimini utekelezaji wake.

Kufahamu hali ya utunzaji wa mazingira  ilivyo nchiniUgandaungana na John Victor Kibego anayeainisha juhudi za  serikali katika kukemea uharibifu wa mazingira nchini humo

Kuelekea ukomo MDGS, elimu ya msingi yaboreshwa Tanzania

Wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukiendelea mjini New York huku mjadala mkuu ukiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia , Tanzania imepiga hatua katika lengo la pili la elimu kwa wote ambapo takwimu zinasema mwaka jana uwiano wa uandikishaji wa wavulana ulikuwa asilimia 14.4  huku wasichana ikiwa aslimia 97.3

Suala la DR Congo na Misri bado ni changamoto kwa jumuiya ya Kimataifa:

Suala la vikundi vya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwemo kundi la M23 na wanamgambo wengine kama Mayi-Mayi na FDLR badi ni changamoto kwa jumuiya ya kimataifa kama lilivyo suala la kupata suluhu ya kisiasa nchini Misri baada ya kupinduliwa Rais Mohammed Morsi. Hayo yamejiri katika mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi kwenye baraza Kuu la Umoja wa mataifa.

Ili kuyachambua kwa undani yaliyojitokeza kuhusu nchi hizo mbili Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ameketi na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernad Membe anayeanza kufafanua kuhusu suala la Congo

Tanzania yapiga hatua kudhibiti vifo vya wajawazito

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDGS ni moja ya agenda muhimu wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa uanotarajiwa kuanza mnamo September 23 mwaka huu mjiniNew York.

Ungana na Tamimu Adam kutoka radio washirika , Jogoo Fm mkoani Ruvuma katika makala inayoangazia namna utekelezaji wa lengo la tano la kupunguza vifo vya wajawazito lilivyotekelezwa nchiniTanzaniakatika mkoa waRuvuma.

Migomo ya elimu iepukwe kunusuru mustakabali wa elimu:UNESCO

Migomo katika sekta ya elimu hudidimiza kiwango cha elimu katika eneo husika na hivyo kuzorotesha maendeleo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO. Katika kuangazia hili afisa wa UNESCO nchini Tanzania Elizabeth Kyondo anasema ni muhimu mazingira ya walimu yakaboreshwa ili wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuleta tija katika mustakabali wa elimu hususani shule ya msingi. Ungana na Joseph Msami pamoja na Victor Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchini Uganda, katika makala inayomulika mgomo wa waalimu wa shule za msingi nchini Uganda na