Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakenya waongea kuhusu walinda amani

Kazi ya walinda amani ina changamoto kubwa, lakini pia faida nyingi. Leo, Mei 29, ulimwengu unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani. Lakini je, raia wa kawaida wanaiona vipi kazi ya walinda amani? Na je, raia hao wangeombwa wajiunge na kazi ya kulinda amani, wangefanya hivyo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo Jason Nyakundi amewauliza watu mitaani mjini Nairobi, Kenya.

Reinada Milanzi: Mlinzi wa amani kutoka Tanzania aliyejikita kujenga uhusiano wa kijinsia katika jamii

Shughuli za ulinzi wa amani ni zaidi ya kuzuia mapigano bali pia kuweka mazingira ambamo kwao uhusiano wa kijamii unaweza kuwa bora na maisha yakasonga mbele, kwani chokochoko za kijamii zinaweza kuwa chanzo cha mapigano ya kivita. Mathalani ukatili wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia unaweza kukithiri katika maeneo ya migogoro lakini pindi amani inapopatikana basi suala hilo nalo lazima lishughulikiwe ili mchakato wa amani usonge mbele.

Twahitaji wataalamu zaidi wa kutibu Fistula: CCBR

Wakati dunia inaadhimisha siku ya kwanza kabisa ya kutokomeza Fistula, jeraha alipatalo mzazi wakati wa kujifungua iwapo anakosa huduma muhimu au maungo yake hayajakomaa kubeba ujauzito, hospitali ya CCBRT nchiniTanzaniainasema bado wataalamu hawatoshi kukidhi mahitaji wakati huu ambapo elimu zaidi inatolewa ili wanawake wenye Fistula waweze kujitokeza kutibiwa jerahahilo. Kauli hiyo ni ya Dokta Robert Marenga, mtaalamu wa kutibu Fistula kwenye hospitali ya CCBRT na alitoa alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini DSM.

Utayari wa wasomali umerahisisha mchakato wa amani- Balozi Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Balozi Augustine Mahiga anahitimisha wadhifa wake huo mapema mwezi ujao baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu.Katika kipindi chakeSomaliailiyokuwa imegubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili imeweza kuwa na serikali, bunge na sasa mchakato wa kujenga miundombinu inaendelea. Katika sehemu hii ya pili ya mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa, Balozi Mahiga anazungumzia kile kilichofanikisha mchakato wa kisiasa.

TEKNOHAMA yabadili mfumo wa biashara kwa wajasiriamali wanawake

Mkutano wa kimataifa wa Jamii Habari wa tarehe 13 hadi 17 Mei huko Geneva, Uswisi ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la mawasiliano, ITU pamoja na mambo mengine unaangalia fursa mpya kwa wajasiriamali wanawake za kuimarisha biashara zao kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano, TEKNOHAMA au ICT kwa kimombo. Mathalani matumizi ya simu za mkononi, mitandao ya kijamii na kadhalika.

Ukatili wa ngono wakabiliwa DRC

Ripoti ya pamoja ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, DRC, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia hususani ni ubakaji nchini humo, inaonyesha kwamba takribani wanawake 200 wamebakwa  katika kipindi cha mwezi November pekee mwaka jana.

Kazi niliyotumwa Somalia nimeimaliza kwa wakati na kwa amani-Balozi Mahiga

Baada ya miaka mitatu ya kuhudumu kama Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema jukumu hilo lilikuwa ni kubwa na changamoto nyingi. Lakini alisonga mbele hadi kuwezesha kuundwa kwa serikali, bunge na katiba nchini humo. Balozi Mahiga ambaye anahitimisha jukumuhilomwezi ujao wa Juni, alisema hayo katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Radio ya  Umoja wa Mataifa ambapo katika sehemu hii ya kwanza anaanza kwa kuzungumzia alivyopokea jukumu hiloJuni 2010.

Tanzania yasema haitishiki na vitisho vya M23

Mwishoni mwa wiki, serikali ya Tanzania ilipata ridhaa ya Bunge la nchi hiyo ya kupeleka vikosi vyake kuungana na brigedi iliyoundwa kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuweka utulivu huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, DRC. Brigedi hiyo itajumuisha pia vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi ambapo imeripotiwa kuwa waasi wa M23 wamedai kuwa Tanzania isipeleke vikosi vyake na ikifanya hivyo itajutia.