Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 NOVEMBA 2023

30 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 ukiwa umefunguliwa rasmi hii leo huko Dubai, utasikia ujumbe wa Ashraf Nyorano Mugenyi mwenye umri wa miaka 80 mkazi wa Hoima nchini Uganda. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwema za ukanda wa Gaza, mabadiliko ya tabianchi na Malaria, na tunakuletea uchambuzi wa methali MWENYE KELELE HANA MANENO.  

  1. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 umefungua pazia rasmi mjini Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu kwa kuwaleta Pamoja wajumbe zaidi ya 60,000 kuangalia jinsi ya kuongeza hatua, fursa ya nyenzo za kujenga mnepo ikiwemo makubaliano ya kuanzishwa mfuko wa hasara na uharibifu ambayo yamepitishwa kwenye mkutano huo na pia kutumia ubunifu kudhibiti janga hilo. 
  2. Tukisalia ma mabadiliko ya tabianchi ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu hali ya hewa duniani na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imethibitisha kwamba mwaka 2023 utavinja rekosi ya kuwa mwaka wenye joto Zaidi katika historia huku shirikika hilo likionya kuhusu mwenendo unaoashiria kutokea kwa mafuriko zaidi, moto wa nyika, kuyeyuka kwa barafuna joto la kupindukia katika siku zijazo.
  3. Na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema katikia ripoti yake mpya iliyotolewa leo kwamba licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kupanua wigo wa kupata vyandarua vya mbu vyenye dawa pamoja dawa za kusaidia kuzuia malaria kwa watoto na kina mama wajawazito, watu wengi wamekuwa wakiugua malaria. Kwa mujibu wa shirika hilo mwaka 2022 kulikuwa na wagonjwa wa malaria milioni 249 duniani kote ikiwa ni wagonja milioni 16 zaidi ya ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19.
  4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MWENYE KELELE HANA MANENO

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
12'20"