Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 NOVEMBA 2023

27 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Gaza, siku ya nne ya sitisho la mapigano; kisha kauli ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kulekea COP28. Makala ni kauli ya muathirika wa mapigano huko Mashariki mwa DRC na mashinani mnufaika wa kilimo endelevu kutoka Kenya.

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza serikali za Qatar, Misri na Marekani pamoja na kutambua jukumu muhimu la kamati ya Kimataifa ya chama cha msalaba mwekudu kwa juhudi zao za kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa muda, mateka na wafungwa wanaachiwa pamoja na kuingiza misaada huko Ukanda wa Gaza.
  2. Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote.
  3. Makala: Evarist Mapesa wa Idhaa hii anafuatilia madhila wanayopitia watu 450,000 waliofurushwa makwao katika kipindi cha wiki sita zilizopita huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojiham.
  4. Mashinani:Leo nampa fursa Hannah Karanja, mkulima mnufaika wa mpango wa kilimo endelevu kinachohusisha utandazaji wa majani makavu kama njia ya kuepusha matumizi ya mbolea zenye kemikali, mradi unaofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'57"