Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 NOVEMBA 2023

24 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza na msaada wa kibinadamu nchini Chad. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani tunamulika Ibara ya 13 ya Tamko la Haki za Binadamu.  

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. 
  2. Chad ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya milioni ambao sasa umekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi na unaokuwa kwa kasi barani Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hilo linasema na vita inayoendelea katika nchi jirani ya Sudan imeongeza shinikizo la rasilimali na mahitaji ya kibinadamu kwani maelfu kwa maelfu ya watu zaidi wanavuka mpaka na kusaka usalama Chad.
  3. Katika makala John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime FM ya Morogogo Tanzania anatujuza kuhusu Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Tanzania unaokusudia kuhamasisha wafugaji wa kuku kupunguza matumizi ya dawa, mathalani za viuavijiumbemaradhi wakati wa ufugaji wa kuku wa nyama nchini humo.
  4. Na mashinani leo katika mfululizo wetu wa uchambuzi wa Ibara za Tamko la Haki za Binadamu kuelekea Siku ya Haki za Binadamu itakayoadhimishwa hapo Desemba 10 leo tunamulika Ibara ya 13

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'