Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 JANUARI 2023

18 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakupeleka Davos Uswisi kusikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia kuangazia tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award. Makala na mashinani tunasalía huko huko, kulikoni?

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.
  2. Mabalozi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya kilimo duniani, IFAD, Sabrina Dhowre Elba na mumewe Idris Elba wamepatiwa tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award kutokana na uongozi wao wa kupaza sauti kwa niaba ya mamilioni ya wakulima wadogo maskini duniani kote ambao hufanya kazi kila siku kuzalisha theluthi moja ya chakula chote duniani.
  3. Makala tunakwenda huko Fez, kuangazia mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC.
  4. Na katika mashinani tunasalia huko nchini Uswisi ambapo tutamsikia Waziri Mkuu wa Finland. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'42"