Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

31 JANUARI 2023

31 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tuakuletea mada kwa kina na tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika kampeni ya chanjo iliyomalizika jana Jumanne.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za afya, haki za binadamu na wakimbizi. Katika mashinani tutakupeleka Geneva nchini Uswisi kupata ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, UNAIDS kuhusu kizazi cha watato ulimwenguni ambao wako hatarini kusahaulika.      

  1. Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wametaka kufanyika mara moja kwa uchunguzi huru nchini Mali kwa kile walichoeleza kuwa ni kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na uwezekano wa uhalifu wa kivita unaosadikiwa kufanywa na vikosi vya serikali kwa kushirikiana na kundi binafsi la wanajeshi la Wagner group.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezindua Baraza la vijana lililofanyika kwa siku nne jijini Geneva Uswisi na kuwaleta pamoja viongozi vijana kutoka mashirika 22 ya vijana duniani yanayojishughulisha na masuala ya afya na masuala yasiyo ya afya lengo likiwa ni kuwasikiliza vijana, kupata utaalamu na uzoefu wao katika masuala ya afya kwa umma pamoja na kufanya nao kazi katika kutengeneza harakati za vijana katika afya.
  3. Na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema kumekuwa na ongezeko kubwa la wakimbizi wa Rohingya wanaowasili Kusini Mashariki mwa Asia kwa njia ya bahari na njia za barabara. IOM imese mwaka 2022 imerrkodi kuwasili kwa watu 3300 nchini Malaysia, Indonesia na Thailand hili likiwa ni takriban ongezeko la asilimia 290 ikilinganishwa na watu 850 waliowasili mwaka 2021.
  4. Katika mashinani tutakupeleka Geneva nchini Uswisi kupata ujumbe wa Charlotte Sector, Msemaji wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu VVU / UKIMWI (UNAIDS) akisisitiza umuhimu nchi za Afrika kuzindua "Muungano wa kimataifa wa Kutokomeza Ukimwi kwa Watoto" katika kanda huo  ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto wachanga 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu !

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'26"