Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 JANUARI 2023

26 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Kenya kuangazia juhudi za mradi wa Teen Seed Africa unavyorejesha matumaini ya elimu kwa wasichana walioacha shule kutokana na mimba za mapema.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini DR Congo, Ethiopia na Senegal. Katika kujifunza Kiswahili   ambapo utapata ufafanusi wa msemo "TABIA NI NGOZI."

  1. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umesema wataalamu wake wa kutegua mabomu na wale wa ofisi ya Umoja huo ya kudhibiti mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS wamefika katika mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini hususan kitongoji cha Macampagne ambako jana Jumatano bomu la kutengenezwa lililipuka kwenye soko na kujeruhi watu 17.
  2. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu, imesema Kamisheni ya Kimatiafa kuhusu haki za binadamu nchini Ethiopia imetambua chapisho la serikali la rasimu ya kwanza ya kisera kuhusu haki kwenya kipindi cha mpito.
  3. Na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO Gilbert F. Houngbo yuko ziarani nchini Senegal,  ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanywa na kiongozi wa shirika hilo nchini humo na anatumia fursa ya ziara yake hiyo ya siku 4 kujadili na mamlaka na vyama vya wafanyakazi mwelekeo wa ajira katika dunia ya sasa hususan ajira yenye hadhi kwa vijana na wanawake, ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji na urasimishaji wa uchumi usio rasmi.
  4. Leo katika kujifunza Kiswahili mtaalam wetu  Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anafafanua maana ya msemo "TABIA NI NGOZI."

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'15"