Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 Januari 2023

23 Januari 2023

Pakua

Hii leo jarida linaangazia afya likikuletewa ripoti kuhusu ugonjwa wa moyo na WHO na, na pia tuanakupeleka nchini Madagascar kuangazia miradi mbalimbali. Makala na mashinani tunakwenda nchini Rwanda, kulikoni?

  1. Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo Jumatatu Januari 23, 2023 imebainisha kuwa watu bilioni tano duniani hawajalindwa dhidi ya viambato hatari vya mafuta vilivyoko katika bidhaa za vyakula vinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kifo.
  2. kupitia mradi wa mabadiliko ya haraka vijijini (RRT) shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wake wameanzisha kituo maalum cha paneli za sola ambacho ni chanzo kikuu na endelevu cha maji na teknolojia ya mawasiliano ICT katika maeneo ya vijijini nchini Madagascar, hatua inayoruhusu upatikanaji wa huduma muhimu kama vile nishati, maji na mitandao ya kijamii kwa wakazi wa jamii hizo na kwa njia inayojali mazingira.
  3. Makala tunakwenda nchini Rwanda kuangalia ni vipi mpango wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa umeleta mabadiliko madarasani nchini humo.
  4. Na katika mashinani tutasalia huko huko nchini Rwanda kumsikia Murekatete Agnes, mtafiti wa kisayansi na mataalam wa maabara  katika maabara ya inayohusika na vyanzo, tiba na kuzuia magonjwa yanayohusiana na damu au Immunohematology. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'33"