17 AGOSTI 2022
Hii leo jaridani tunaanzia Yemen ambako shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limepeleka misaada ya vifaa vya matibabu kwa ajili ya manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo. Kisha ni Pembe ya Afrika wanawake na watoto wakiwa katikati ya kukumbwa na janga la njaa wanakumbuka hali ilivyokuwa bora kabla ukame haujatumbukiza maisha yao kwenye hali tete. Makala tunabisha hodi mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako huko wataalamu wanafafanua maana ya sumu kuvu na athari zake kiafya na kwenye mazao.