Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 AGOSTI 2022

10 AGOSTI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaanza na sarafu za kidijitali au Cryptocurrency kwa kiingereza ambapo Umoja wa Mataifa unatoa kuwa inatishia utulivu wa kifedha kutokana na ukosefu wa será za udhibiti na usimamizi. Sasa kupitia UNCTAD, UN inatoa miongozo ya kisera. Kisha tunakwenda Kenya huko ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limepatia watu 62 cheti cha kuhitimu mafunzo ya stadi ambazo walikuwa wamebobea bila mafunzo rasmi, sasa wanakwambia “sisi juakali tunaweza kuomba zabuni hata serikalini.” Mashinani tunasalia Garissa nchini Kenya kwenye mradi wa maji na makala tunakwenda Uganda kwa wakimbizi wanufaika wa miradi ya kuwapatia kipato badala ya kusubiri misaada. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'59"