Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 AGOSTI 2022

08 AGOSTI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaanza na habari kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto na tunakwenda Morogoro nchini Tanzania. Kisha tunamulika harakati za FAO kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo ili waweze kupanda mazao msimu huu wa Meher na kisha wavune Oktoba mwaka huu. Makala tunamulika kijana Suzan Yumbe na taasisi yao ya Afya Plus Tanzania na changamoto alizokumbana nazo kuelekea kuanzisha shirika hilo. Mashinani tunasalia Tanzania na ujumbe wa kijana Hussein Meleke kwa  vijana wa Kenya wanapokwenda kupiga kwenye uchaguzi mkuu kesho Agosti 9. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'38"