Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 AGOSTI 2022

04 AGOSTI 2022

Pakua

Hii leo jaridani kubwa ni mada kwa kina ikitupeleka nchini Kenya ambako mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Thelmwa Mwadzaya ametembelea shule inayosomesha watoto wa kike bila malipo, watoto ambao wako hatarini kukumbwa na ndoa za utotoni na ukeketaji au FGM. Nini kinfanyika? Na wazazi wanasemaje? 
Katika habari kwa ufupi Leah Mushi anamulika habari njema za kuongezeka kwa umri wa kuishi maisha tena kwa afya barani Afrika, kiwango ambacho hakijafikiwa na ukanda wowote wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO. Tunataja pia washindi kutoka Afrika wa shindano la mbinu bunifu za kuwezesha na kuinua wanawake na wasichana likimulika zaidi afya ya uzazi na idadi ya watu na mwisho ni miaka miwili tangu mlipuko huko Beirut, Lebanon.
Kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tukipata msemo hakuna Congo bila Beni! Kulikoni? Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'24"