Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 17 Agosti 2021

Katika jarida na Grace Kaneiya hii leo utasikia kuhusu msaada unaotolewa na shirika la FAO kwa wananchi wa Afghanistan. Pia utasikia mkimbizi wa Syria aliyeko nchini Libya na Makala ni kuhusu ufugaji wa nzi. 

Sauti
12'34"

Jarida 16 Agosti 2021

Karibu usikilize Jarida ambapo leo kwenye Muhtasari wa habari utasikia kuhusu
- Baraza la usalama ambalo limekutana katika mjadala wa wazi kujadili hali inavyoendeea nchini Afghanistan.
-watoto wameanza kurejea shuleni nchini nchini Palestina 
- Hali nchini Haiti huwenda kuwa mbaya zaidi leo usiku
Na katika mada kwa kina tunaenda nchini Tanzania  kufuatilia ziara ya mafunzo ya wakulima kutoka mkoani Kigoma kwenda Kagera, ziara iliyoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO. 

Sauti
11'54"

13 Agosti 2021

Jaridani Agosti 13, 2021 

Katika Jarida la leo Ijumaa tuna habari muhimu kwa siku ikiwemo hali ya kusikitisha ya ongezeko la vitendo vya ukatili wa kingono nchini DRC pia hali tete nchini Afghanistan. Aidha visa vya saratani barani Afrika vimeongezeka. 

Mada yetu kwa kina inamwangazia mwandishi wa habari nchini Tanzania aliyezushiwa kufariki kutokana na COVID-19.

Katika neno la wiki ni uchambuzi we methali heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi.

Sauti
11'36"

12 Agosti 2021

Ikiwa leo ni siku ya vijana duniani, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuimarisha mifumo ya chakula duniani kwa kuzingatia kuwa miaka 30 ijayo watu bilioni 2 zaidi wataongezeka duniani na kuongeza mahitaji ikiwemo ya chakula.

Nchini Zambia wanufaika wa mradi wa kuimarisha lishe au SUN ulioanza mwaka 2014 wamepaza sauti zao wakielezea jinsi watoto wao wameimarika kiafya na wakati huo huo kipato cha familia kuongezeka.

Sauti
12'11"

11 Agosti 2021

Jaridani Agosti 11, 2021-

Mkimbizi wa ndani kutoka Tambura asimulia alivyotakwa sikio na kutakiwa kulila

Kutoka mfungwa hadi mkufunzi gerezani: Asante MINUSCA

Masoko maalumu ya kimkakati nchini Tanzania yana mchango chanya katika mifumo ya chakula - FAO

Sauti
12'59"

10 Agosti 2021

Jaridani Jumanne Agosti 10, 2021 na Assumpta Massoi-

Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake wamepata tena uwezo wa kuingia katika kambi za wakimbizi za Mai Aini na Adi Harush zinazohifadhi wakimbii wa Eritrea nchini Ethiopia.

Mradi wa pamoja Kigoma unaoendeshwa kwa pamoja na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo, FAO umezidi kuwajengea kujiamini wakulima kwa kuwa hivi sasa kilimo chao kinahimili mabadiliko ya tabianchi na kiwango cha mavuno kimeongezeka bila uchovu ikilinganishwa na awali.

Sauti
14'12"

09 Agosti 2021

Jaridani Agosti 9, 2021-

Ungana na Assumpta Massoi katika jarida likiangazia habari muhimu kwa siku na pia makala yetu ya wiki imejikita katika siku ya jamii ya watu wa asili ambayo imekwenda nchini Kenya. Pia kutoka mashinani ni uhifadhi wa mbegu za asili nchini Zimbabwe.

Sauti
9'28"

6 Agosti 2021

Jaridani Agosti 6, 2021 na Assumpta Massoi,

Jarida linaanza na habari muhimu za siku, kisha mada kwa kina kutoka Uganda ambapo utasikia simulizi ya mwanamke aliyepata COVID-19 na kupona, alipata matunzo ya wiki mbili akidhani anaumwa malaria, kulikoni?

Sauti
11'52"

5 Agosti 2021

Jaridani Agosti 5, 2021 na Assumpta Massoi-

Heko China kwa kuchangia dozi milioni 500 za COVID-19: UN

Mbinu mbadala za kipato zanusuru maeneo oevu Uganda

UNICEF na KOIKA wametupatia furaha kwa kutuletea maji Turkana

Sauti
13'42"

04 Agosti 2021

Jaridani Jumatano Agosti 4, 2021

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Kenya linaendesha programu ya majaribio ya kutumia roboti ili kupima afya za wasafiri wanaoingia na kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, pamoja na Hospitali Kuu ya Taifa ya Kenyatta.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na wadau wake kama shirika la LIXIL na FINISH INK ya nchini humo, wanatoa mafunzo na ufadhili kwa wajasiriamali wachanga hasa wanaojiuhusisha na miundombinu ya usafi na kujisafi.

Sauti
12'45"