Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 Agosti 2021

10 Agosti 2021

Pakua

Jaridani Jumanne Agosti 10, 2021 na Assumpta Massoi-

Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake wamepata tena uwezo wa kuingia katika kambi za wakimbizi za Mai Aini na Adi Harush zinazohifadhi wakimbii wa Eritrea nchini Ethiopia.

Mradi wa pamoja Kigoma unaoendeshwa kwa pamoja na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo, FAO umezidi kuwajengea kujiamini wakulima kwa kuwa hivi sasa kilimo chao kinahimili mabadiliko ya tabianchi na kiwango cha mavuno kimeongezeka bila uchovu ikilinganishwa na awali.

Wanawake wa jamii ya asili katikati ya msitu wa hifadhi wa Imacata nchini Venezuela wamechukua jukumu la kulinda ardhi yao iliyoathiriwa kwa miaka mingi kutokana na shughuli za madini na ukataji miti. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula

FAO limeunga mkono juhudi za wanajamiii hao kwa kutoa miche ya kurejesha uoto wa asili.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
14'12"